Baada ya tetesi kwamba Deus Kaseke huenda akaungana na kocha Hans van Pluijm pamoja na Tafadzwa Kutinyu kutoka Singida United kujiunga Az...


Baada ya tetesi kwamba Deus Kaseke huenda akaungana na kocha Hans van Pluijm pamoja na Tafadzwa Kutinyu kutoka Singida United kujiunga Azam, mkurugenzi wa Singida United amesema Kaseke atatimkia South Afrika ambako amepata ofa.
Festo Sanga amekanusha taarifa za muda mrefu ambazo zimekuwa zikimhusisha Kaseke kujiunga na Azam kutokana na uhusiano wake mzuri na Hans van Pluijm ambaye ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.
“Deus Kaseke amepata ofa kutoka South Afrika, kuna timu imepanda ligi kuu ya huko inamuhitaji Kaseke. Sina taarifa kwamba anakwenda kuungana na kocha Hans”-Festo Sanga.
Kaseke alijiunga na Yanga wakati Pluijm akiwa kocha mkuu wa ‘timu ya wananchi’ wawili hao wakaungana tena Singida United inawezekana ndiyo sababu ya kuhusishwa tena kutaka kufanya kazi pamoja Azam FC.

Inasemekana timu ya taifa ya Argentine imefutilia mbali mchezo wao wa kirafiki dhidi ya taifa la Israel. Taifa hilo lilipata ripoti kwamba...


Inasemekana timu ya taifa ya Argentine imefutilia mbali mchezo wao wa kirafiki dhidi ya taifa la Israel. Taifa hilo lilipata ripoti kwamba Lionel Messi na mke wake walipokea vitisho kutoka kwa wapalestine wakiwataka kuahirisha mchezo huo mara moja.

Katibu mkuu wa chama cha soka cha Palestina Jibril Rajoub aliuomba uongozi wa chama soka cha argentine kufuta mchezo huo mara moja

Baadhi ya mashabiki wa Messi nchini Palestina walichoma jezi za nyota huyo mara baada ya kikosi hicho kuwasili Jerusalem kwa muda.

Rajoub amesema anafahamu wazi kuwa mchezo huo ulikuwa ni wa kusheherekea Miaka 70 ya shirikissho la soka nchini humo.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwasiliana na Rasi wa Argentine Mh Mauricio Macri. Netanyahu alimsihi Sana Macri kuwahimiza uongozi na wachezaji kutokufutilia mbali mchezo huo siku ya jumanne. Macri alimjibu waziri huyo kuwa yeye hawezi kuingilia maamuzi ya mwisho ya chama cha soka cha taifa hilo.

Raisi Macri aliwasiliana na uongozi wa chama cha soka kujua msimamo wao. Viongozi walimwambia kuwa kila mchezaji ana hofu na hakuna mchezaji ambaye yupo tayati kucheza pambano hilo. Macri alimpigia simu waziri wa Israel na kumuomba radhi kwamba hakuna mchezaji ambaye atakubali kucheza pambano hilo.

Macri mwenyewe alikuwa tayari kwenda katika mpambano baada ya kualikwa na matajiri wa kiyahudi wanaofanya kazi.

Mchezaji wao Gonzalo ” Nashukuru kwa maamuzi hayo Kwa ajili afya zetu na maisha yetu. Hakukua na haja ya kucheza na wayahudi.

Hata hivyo Uongozi wa chama cha soka cha Israel kimishtumu sana maamuzi ya Rajoub na kusema amevunja mipaka.

Waziri wa Ulinzi wa israel Avigdor Lieberman amelaani kitendo hicho na kudai kuwa Wapalestina wamejaa chuki na wivu.

Msemaji wa wizara ya ulinzi Gilad Erdan alionhelea suala hilo na kusema kwamba

wamekuza jambo hilo kwa makusudi ili kumtisha Messi. Amesema kitendo cha kuchoma jezi za nyota huyo ni mipango ya taifa hilo kutaka kuondoa amani.

Kocha mfaransa wa Simba Pierre Lechatre amebakiza siku 43 kwenye mkataba wake wa kuifundisha Simba. Mkataba wa Lechatre utamalizika June ...


Kocha mfaransa wa Simba Pierre Lechatre amebakiza siku 43 kwenye mkataba wake wa kuifundisha Simba.

Mkataba wa Lechatre utamalizika June 18, 2018 ambapo atakuwa huru kuondoka au kubaki Simba kama watahitaji kuendelea nae.

Haji Manara akiwa Kenya amethibitisha kwamba mkataba wa kocha wao unaelekea ukingoni na amewaomba wanasimba kuwa watulivu na wavumilivu wakisubiri uongozi uamue kama utaendelea au utaachana na kocha huyo.

“Kocha Lechantre mkataba wake unamalizika mwezi June 18, 2018 uongozi utakaa nae utaona kama ipo haja ya kuendelea nae au la”-Haji Manara.

Lechantre alisaini mkataba wa kuifundisha Simba katikati ya msimu akichukua nafasi ya Joseph Omog ambaye alitimuliwa.

Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Singida United kupitia kwa Rais wake, Mwigulu Nchemba, umempanga kumtumia tiketi mshambuliaji wa kimata...


Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Singida United kupitia kwa Rais wake, Mwigulu Nchemba, umempanga kumtumia tiketi mshambuliaji wa kimataifa kutoka Benin, Marcellin Koukpo ambaye alitajwa kutua Yanga.

Singida wameingia kwenye rada na mshambuliaji huyo ambaye ilielezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na mabingwa mara 27 wa ligi kuu bara, Yanga.

Taarifa zinasema kuwa Singida wamepanga kumtumia tiketi ya ndege ili kumuwezesha Koukpo aweze kutua hapa nchini tayari kumalizana naye mapema ili aanze kuitumikia klabu hiyo.

Wakati Singida wakitaka kuiharibia Yanga mipango hiyo ya usajili wa mchezaji huyo, uongozi wake kupitia Boniface Mkwasa umekuwa ukilalamika kuhusiana na kuchukuliwa wachezaji wake ambao wamekuwa wakiwataja ili waweze kuwasajili.

Kitendo hicho kilimuibua Mkwasa na kueleza kuwa hawatothubutu kuweka wazi nani na nani wanataka kusajili na badala yake watafanya kimyakimya ili kuzinyima nafasi timu ambazo zimekuwa zikiwaibia wachezaji hao.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa tim...


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Rajabu Digongwa aliyefariki huko mkoani Tanga.

Rais wa TFF Ndugu Karia amepokea kwa huzuni na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha mchezaji huyo wa zamani aliyefariki baada ya kuugua.

Kwa niaba ya TFF Rais wa TFF Ndugu Karia ametoa pole kwa familia ya mchezaji huyo ,wanafamilia wa Mpira wa Miguu,ndugu ,jamaa na marafiki.

“Marehemu Digongwa namfahamu vizuri toka enzi akicheza na kifo chake kimenishtua na kunihuzunisha kwa niaba ya TFF natoa pole kwa wafiwa" alisema Karia.

Enzi za uhai wake marehemu Digongwa alicheza timu za Wananchi FC, African Sports, pia alipata kuitwa kwenye timu ya mkoa wa Tanga na pia timu ya Taifa ya Tanzania.

 Mazishi ya marehemu Digongwa yamefanyika leo saa 4 asubuhi mkoani Tanga

Wakati huohuo Rais Karia pia ametuma salamu za rambirambi kwa mchezaji wa zamani Khalid Bitebo aliyefiwa na mkewe.

Ametoa pole kwa Bitebo na familia kiujumla akiwataka kuwa na subira katika kipindi hiki cha majonzi. 

  Elizabeth lyavule zimesalia siku tisa tu mataifa 32 yakianza kuoneshana ubabe kombe la dunia, huku macho ya wengi wakingojea kumuona...

 


Elizabeth lyavule
zimesalia siku tisa tu mataifa 32 yakianza kuoneshana ubabe kombe la dunia, huku macho ya wengi wakingojea kumuona Marcus Rashford na Uingereza, Marco Asensio na Hispania, Paul Dybala wa Argentina na wengine wengi, jaribu kuwafumbia macho hawa tuliowazoea na uwacheki makinda hawa tusiowajua sana na kuwasifu uwezo wao kule Urusi.
Hirving Lozano raia wa Mexico. Alianza maisha yake ya soka kama mshambuliaji nchini kwao Mexico akiwa na klabu ya Pachuka, msimu wake wa kwanza alifunga magoli 18 ndani ya michezo 37 aliochezea klabu yake hivyo maskauti wa timu ya PSV nchini Uholanzi walimuona wakamsajili na akiwa PSV amemaliza msimu akiwa ni mfungaji bora wa klabu magoli 17 na mfungaji namba tano wa ligi ya uholanzi pia alifanikiwa kutoa pasi za mwisho zilizozaa magoli 9 kubwa zaidi kaisaidia PSV kuwa mabingwa wa uholanzi (eredvisie).

Ana uwezo mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa, ana krosi nzuri na katika umri wake wa miaka 22 aliitwa timu ya taifa Mexico na mchezo wake wa kwanza ilikua mwezi wa pili mwaka 2016 dhidi ya Senegal alifanikiwa kutoa pasi ya goli katika mechi hiyo. Ana magoli 7 katika michezo 26 aliyoichezea nchi yake moja akiifunga timu ngumu ya ubeligiji mwezi wa 11 mwaka 2017 katika sare ya goli 3-3. Ana uhakika wa namba Mexico tuone ataunda vipi ushirikiano na wenzie kuifanya nchi yao ifike mbali mwaka huu kule Urusi.

Lucas Torreira wa Uruguay ni kinda mwenye miaka 22 anaetizamiwa kuwa na mashindano mazuri ya kombe la dunia Urusi. Anacheza kama kiungo mkabaji na sasa yupo katika klabu ya Sampdoria nchini Italia, msimu uliokwisha amecheza michezo 33 ya ligi ya Italia “seria a” ametengeneza nafasi 33 za kufunga, akiingilia mpira kwa mpinzani (interception) mara 67 pia akifanikiwa kumpora mpira mpinzani (tackling) mara 66 si kitu kidogo kwa umri wake. Kwa takwimu hizo haitakua ajabu kumuona akiunda kikosi cha kwanza na wakali wengine kama Diego Godin, Suarez, Edson Cavan nakuifikisha mbali nchi yake katika mashindano hayo.
Aleksandr Golovin wa Urusi. Akiwa ni mwenyeji kinda huyu mwenye miaka 22 atapambana vilivyo kuiokoa nchi yake kukwepa aibu yakutoka mapema, anacheza katika klabu ya CSKA Moscow ya urusi na ni mmoja kati ya wachezaji waliobeba kombe la Ulaya la vijana chini ya miaka 17 mwaka 2013,

kinda huyu ni kiungo wa kati anaeweza kuunganisha timu kati ya ulinzi na ushambuliaji (box to box midfielder) huku akisifika kwa uwezo mkubwa wa kukokota mpira, kutoa pasi nzuri na kukaa na mpira bila adui kumpokonya.

Amecheza mechi 38 mashindano yote msimu wa 2017-2018 akafunga magoli 7, akatoa pasi za kufunga 4 si kitu cha kubeza kwa umri wake.
Ismaila Sarr raia wa Senegal. Kinda huyu wengi wanamlinganisha na Sadio Mane na wanamtabiria kufanya vizuri kuliko Sadio Mane akikomaa mana ndio kwanza ana miaka 22 tu.

Anacheza nafasi ya ushambuliaji kutokea pembeni huko Ufaransa katika klabu ya Rennes na msimu wake wa kwanza alikua na goli 5 pasi za mwisho zilizozaa magoli 5 katika michezo 22 aliyoanza huku 2 akitokea benchi. Akiwa na Senegal mwezi wa 9 mwaka 2016 alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Namibia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Sadio Mane.

Kwasasa kashacheza michezo 10 nakufanikiwa kupata magoli 2. Ataungana na washambuliaji wengine kama Mame Biram Diouf, Maussa Sow, Diafra Sakho na Sadio Mane kuhakikisha wanaiwakilisha vizuri Senegal na Africa kiujumla wafike mbali.

Cristian Pavon kinda kutoka Argentina. Winga huyu hategemewi sana kupata nafasi kutokana na upinzani wa nafasi anayocheza kujaa wachezaji wazuri wenye vipaji kama Angel Di Maria, Paul Dybala na mfalme Leonel Messi.

Anacheza nchini kwao Argentina katika klabu ya Boca Junior,kawa na msimu bora ulopita akiifungia klabu yake magoli 6 nakutoa pasi 11 za mwisho zilizozaa mabao nakumfanya kocha Sampaoli kumuita kikosi cha wachezaji 23 watakaoiwakilisha nchi kombe la dunia,

aliichezea Argentina dhidi ya Urusi mwaka uliopita na kufanikiwa kutoa pasi iliozaa goli pekee lililofungwa na Sergio Kun Aguero katika ushindi wa 1-0 waloupata pia alitoa pasi kati ya magoli mawili katika mchezo wa kirafiki waliopoteza dhidi ya Nigeria.

Macho ya vilabu vyote vikubwa barani Ulaya yatakua Urusi kucheki vipaji kama hivi na haitakua ajabu kusikia wameenda timu kama Manchester utd, Arseno na Napoli pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa majira haya ya kiangazi.

  Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amekanusha taarifa inayosambaa kwenye social media kwamba amejiuzulu kuifundisha klabu hiyo ambayo...


 
Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amekanusha taarifa inayosambaa kwenye social media kwamba amejiuzulu kuifundisha klabu hiyo ambayo kwa sasa ipo nchini Kenya ikiendelea na mashindano.
Kocha huyo amesema hawezi kuondoka Simba hadi akamilishe kilichompeleka.
“Sijajiuzulu, maneno hayo siyajui ninamkataba Simba na nimepanga kumaliza mkataba wangu kwa amani, mimi nipo hadi nihakikishe nimefanya kilichonileta Simba”-Masoud Djuma.
Click ‘play’ hapa chini usikilize sauti ya Masoud Djuma alivyokanusha story inayo-trend kwenye social media kwamba ameikacha Simba.

ONLINE USERS